Mfanyakazi wa Acacia Akamatwa Airport Dar Akiondoka Nchini

Mfanyakazi wa Acacia Akamatwa Airport Dar Akiondoka Nchini

491
0
SHARE

Kampuni ya Acacia imesema kuwa mmoja wa wafanyakazi wake wa kimataifa anayefanya kazi na Pangea Minerals Limited amezuiwa kuondoka Tanzania leo Julai 28 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) majira ya asubuhi.

 

Acacia wameeleza kuwa, mfanyakazi huyo ambaye hawakumtaja jina alikamatwa na hati yake ya kusafiria ilichukuliwa huku na yeye akishikiliwa kwa muda.

Kupitia taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti rasmi ya kampuni hiyo, Acacia wamedai kuwa baada ya kuingilia sakata hilo kisheria, mfanyakazi huyo aliachiwa na hati yake ya kusafiria ikarejeshwa.

 

Aidha, wamesema tukio hilo limetokea kipindi ambacho kwa takribani siku mbili sasa wafanyakazi wake wamekuwa wakisumbuliwa na maafisa mbalimbali wa serikali.

Kuhusu tuhuma hizo, serikali kupitia kuwa Msemaji Mkuu, Hassab Abas imesema kuwa inafuatilia tuhuma hizo na baada ya muda mfupi watatoa taarifa kamili.

 

“Tunafuatilia ukweli wa madai ya Acacia kuwa mmoja wa maafisa wake amezuiwa kuondoka Tanzania.Tutatoa taarifa ya kina,” uliandika ukirasa rasmi wa Twitter wa Msemaji Mkuu wa Serikali.

NO COMMENTS