WALICHOKIFANYA WASANII KWENYE TAMASHA LA CASTLE LITE UNLOCKS LEADERS

WALICHOKIFANYA WASANII KWENYE TAMASHA LA CASTLE LITE UNLOCKS LEADERS

333
0
SHARE

TAMASHA la Castle Lite Unlocks lililofanyika katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar  usiku wa kuamkia leo wasanii wa ndani ya Tanzania  na nje waliandika historia kwa kupiga shoo kali wakiongozwa na msanii Futurekutoka Marekani na Refiloe Maele Phoolo ‘Cassper Nyovest’ kutoka Afrika Kusini.

Mashabiki walijitokeza kwa wingi katika viwanja hivyo huku wakimshangilia kila msanii aliyekuwa akipanda stejini kutoka shoo hiyo ya aina yake iliyoandaliwa kwa mbwembwe nyingi.

Wasanii waliofanya shoo katika tamasha hilo  ni: Weusi, Vee Money, Navy Kenzo, Rosa Ree, Cassper Nyovest kutoka Afrika Kusini na msanii kutoka Marekani, Future, na wengineo.

Kundi la Navy Kenzo wakifanya shoo.

Vanessa Mdee ‘Vee Money’ akifanya yake na wacheza shoo wake.

Msanii kutoka Afrika Kusini, Cassper Nyovest, akiongea na mashabiki.

Mashabiki waliofurika katika tamasha hilo.

NO COMMENTS