PM: Siku hizi wazee wapo ‘shapu’ kuliko vijana

PM: Siku hizi wazee wapo ‘shapu’ kuliko vijana

436
0
SHARE

Rais John Magufuli amesema wanaowapa mimba wanafunzi hawana budi kufungwa miaka 30 ili kukomesha suala hilo na kuwapa fursa watoto wasome kwani hao ndiyo viongozi wa kesho.

Akizungumza leo Julai 23 wakati wa uzinduzi wa barabara Kaliua, mjini Tabora, Rais Magufuli amesema wanaowapa mimba watoto wa shule si vijana pekee bali wapo wazee pia.

“Wazee siku hizi wapo shapu kuliko vijana, wanawapa mimba wanafunzi, muwaache wasome, ukimpa mimba mwanafunzi unafungwa miaka 30 nguvu zako zikaishie gerezani,” amesema na kuwataka wanafunzi kusoma ili watimize ndoto zao.

“Soma kwanza, usipate mimba ukiwa shule, subiri umalize sekondari ndipo upate mimba,” amesema.

NO COMMENTS