Nay wa Mitego Ahamishiwa Sentro Dar, Huenda Akapandishwa Mahakamani!

Nay wa Mitego Ahamishiwa Sentro Dar, Huenda Akapandishwa Mahakamani!

703
0
SHARE

DAR ES SALAAM: Rapper Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ jana jioni alihamishiwa katika Kituo cha Kikuu cha Polisi (Sentro) jijini Dar es Salaam kutoka Mvomero, Morogoro alikokuwa anashikiliwa na polisi kuanzia asubuhi ya Jumapili, Machi 26 kutokana na kuachia wimbo unaodaiwa kuwa una maneno ya kichochezi na kuikashfu serikali iliyoko madarakani.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Wakili Peter Kibatala aliandika;

Taarifa nyingine zimeeleza kuwa, Wakili Peter Kibatala naye amejitolea kumtetea bure Nay wa Mitego endapo atapandishwa mahakamani.

Awali, taarifa ya Jeshi la Polisi mkoani Morogoro ilieleza kuwa walianza kumsaka Nay wa Mitego baada ya kuarifiwa kuwa ametimkia, Dodoma, na baada ya kumkamata walitakiwa kumrudisha Dar es Salaam ambako niko lipo shauri la kesi yake.

Kwa upande wao Baraza la Sanaa Tanzania, BASATA wamedai kuwa wimbo alioutoa Nay hivi karibuni ‘WAPO’ hauna maadili na una maneno ya kichozchezi.

NO COMMENTS