Gwajima Azidi Kukomaa na Vyeti vya Makonda

Gwajima Azidi Kukomaa na Vyeti vya Makonda

801
0
SHARE

DAR ES SALAAM: Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima lenye makao yake makuu Ubungo-Maji, Dar, Dk Josephat Gwajima, jana akiwa anaendesha misa kanisani kwake mbele ya waumini wake, ameendelea kukomaa na suala la vyeti na elimu ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Huku akitamba kuwa na ushahidi wa kutosha kuanzia shule ya msingi aliyosoma Makonda ya Koromije kuanzia darasa la kwanza hadi la nne kisha kuhamia Nyegezi na Sekondari ya Pamba kabla ya kujiunga na Chuo cha Uvuvi cha Nyegezi (Mwanza), Mbegani (Bagamoyo) na Chuo cha Ushirika, Moshi, Gwajima alisema kuwa, anashangaa kusikia kiongozi huyo yupo nchini Afrika Kusini kwa pasipoti yenye jina lisilo lake.

“Watu wanasema kwa nini nalipa kisasi, silipi kisasi, namwambia Magufuli amtafutie kazi nyingine ya mtu aliyepata kidato cha nne.

“Namsubiri aje ajibu haya ninayoyasema ndipo nitoke na ushahidi mwingine, nina ushahidi wa kutosha na wote tuseme Amina!

“Hii inaitwa single touch, double manifestation, akijibu moja mimi najibu mbili hadi hapo atakapotoa ushahidi na mimi nitoe wangu,” alisema Gwajima akishangiliwa na waumini na kuongeza:

“Makonda anatakiwa amuombe radhi Magufuli (Rais John Pombe) kisha aliombe msamaha Kanisa la Mungu.”

Kwa wiki ya tatu sasa, Gwajima amekuwa akimuandama Makonda mara tu baada ya kumtaja kwenye orodha ya watu wanaohusishwa na dawa za kulevya huku kiongozi huyo akidaiwa kuwa nchini Afrika Kusini kikazi.

NO COMMENTS