Johari, Chuchu Kimenuka Tena!

Johari, Chuchu Kimenuka Tena!

564
0
SHARE

Warembo wa Bongo Movies, Blandina Chagula ‘Johari’ na Chuchu Hans wamedaiwa kuwa wametibuana vibaya kufuatia Chuchu kumchokonoa Johari mitandaoni kuhusu jina la Kampuni ya RJ, Risasi Jumamosi  linakupa ubuyu kamili.

Chanzo makini kilicho karibu na wawili hao, kimeeleza kuwa, Chuchu amemchokonoa Johari kwa kutupia picha mtandaoni na kuitangaza muvi ambayo  imezalishwa na Kampuni ya RJ inayomilikiwa na mpenzi wa sasa wa Chuchu, muigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ na mpenzi wa zamani wa Ray, Johari kuwa Johari, Chuchu kimenuka tena! imezalishwa na kampuni mpya ya Ray na mwanaye aliyoiita Rjaden (akimaanisha Ray na mwanaye aliyezaa na Chuchu aitwaye Jaden).

Johari

“Johari alimaindi kweli baada ya kusikia Chuchu amebadilisha jina la kampuni na kuita kampuni hiyo jina la mtoto wake. Hakupendezwa na hivi ninavyokwambia wakikutana ni ama za Johari ama za Chuchu. “Johari ameanza kuona kuna mipango ya kutaka kumuondoa jina lake katika kampuni na kubadilisha kisanii jambo ambalo hawezi kukubaliana nalo maana si unajua wamechuma Ray na Johari kwa muda mrefu sana, wamepitia mambo mengi,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:

“Huwezi amini Johari wa watu yupo nyumbani akitafakari cha kufanya maana anaona kuna mchezo anataka kuchezewa.” Hata hivyo, baada ya Chuchu kuweka posti hiyo, chanzo hicho kilieleza kuwa alishambuliwa vibaya na wafuasi wa Johari ambao hawakupendezwa na jambo hilo. “Walimtukana kweli. Waliona ana mipango mibaya. Si unajua tena mihemko ya mashabiki, ilikuwa ni kazi kwelikweli,”kilisema chanzo.

Chuchu Hans

Baada ya kutonywa na chanzo ubuyu huo, Risasi Jumamosi lilimvutia waya Chuchu na kumuuliza kulikoni hadi awe chanzo cha ugomvi huo kutokana na kauli yake aliyoandika mitandaoni na kama kweli ana mpango wa kumzunguka Johari, Chuchu alijibu kwa kifupi na kukata simu. “Hamna kitu kama hicho,” alisema Chuchu.

Chuchu Hans na mpenzi wake Ray

Kwa upande wake Johari, alipoulizwa na mwanahabari wetu na kuelezwa kuwa ameingia kwenye vita mpya na Chuchu ambaye amefuta jina lake katika utambulisho wa kampuni, Johari alikiri kuiona posti hiyo. “Nimeiona posti hiyo mtandaoni na nikwambie tu kuhusu la kuchezewa mchezo, siwezi kukubali kufanyiwa mchezo wowote mbaya… mimi kwa sasa nipo nyumbani namuuguza mama yangu lakini nikienda ofisini na kukuta kitu cha tofauti, nitajua cha kufanya,” alisema Johari.

Wawili hao, awali waliwahi kuingia kwenye malumbano kutokana na kitendo cha Ray kutembea na Chuchu na kumuacha Johari ambaye walitoka naye mbali. Hata hivyo wawili hao wameendelea kufanya kazi pamoja kupitia kampuni yao ya RJ ambayo ipo nyumbani anapoishi Ray na mama’ke,  Sinza-Mori jijini Dar.

NO COMMENTS