Hivi Ndivyo Corner Bar Ilivyofungwa

Hivi Ndivyo Corner Bar Ilivyofungwa

483
0
SHARE

AGIZO la mkuu wa Wilaya ya Kinondini Mkoani Dar es salaam Ali Hapi, kuzitaka baa zote zilizopo ndani Wilaya ya Kinondoni zinazojihusisha na Biashara ya machangudoa kufungwa, Corner Baa ya Sinza Mori Jijini Dar es Salaam imefungwa kwa sasa.

Ametoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa kata ya Kijitonyama waliodai kuwa kuna baadhi ya baa zimekuwa zikiwahifadhi wanaouza miili, hali ambayo ni hatari kwa mazingira na makuzi ya watoto.

“Tutashughulika na changudoa na tutashughulika na wenye baa zinazowahifadhi machangudoa, kwa sababu hili ni suala lililo kinyume cha sheria, serikali inapambana na hili tatizo halafu mwingine analikumbatia, hilo haliwezekani, tutawachukulia hatua za kisheria,” amesema.

 

Awali, akitoa malalamiko yake kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya Sekondari ya Mama Salma Kikwete, mkazi mmoja wa Kijitonyama alidai kuna baa zilizogeuka kero kwao.

NO COMMENTS